Watoa mada toka kushoto: Dr. Subira Samwel, Dr(Sr). Rosamystica Sambu na Dr. Lina Kilumbi (hayupo pichani) wakijiandaa kutoa elimu kwa wasichana wa shule ya Sekondari ya St. Joseph Seminary iliyopo Jijini Mwanza.
Wasichana 355 wamepatiwa mafunzo kuhusu taaluma ya tiba ya wanyama kama sehemu ya uzinduzi wa Siku ya Afya ya Wanyama Duniani ambayo Maadhimisho yake yatafikia Kilele tarehe 29 April, 2023.
Maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa Jijini Mwanza na kumbatana na utoaji wa elimu na huduma za afya ya wanyama kwa Makundi Mbalimbali pamoja na maonyesho ya technolojia na huduma za afya ya wanyama.
Huduma zote zitakazoambatana na maadhimisho onyesho hayo ambayo yatafikia kilele na kuhitimishwa katika viwanja vya Furahisha Kirumba Jijini Mwanza siku ya tarehe 29 Aprili mwaka huu zitatolewa bure kwa wananchi wa makundi yote.
Maadhimisho hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa, wadau mbalimbali wa Mifugo na Wanyamapori pamoja na wananchi wote toka maeneo mabalimbali Duniani na Tanzania.